LATRA NA DART WATOA UFAFANUZI NAULI MABASI YA MWENDOKASI, HAIHUSIANI NA MATUKIO YA OCT 29
Dec 17, 2025•Channel
AI Analysis
Data from YouTube Data API v3•Updated Just now
Video Overview
Video Details
Published5 months ago
Duration6:04
Video ID1dr4Q1sII7A
Languagesw
CategoryNews & Politics
PrivacyPublic
Made for KidsNo
Video TypeRegular Video
Performance Metrics
Views3K
Likes17
Comments26
Engagement Rate1.46%
Likes per 100 views0.58
Comments per 1K views8.81
Description
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Dkt. Habibu Suluo na Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Said Tunda wamefafanua kuhusu nauli mpya inayotumika kwa sasa na Mabasi Yaendayo Haraka ambapo abiria hukatwa shilingi Elfu Moja badala ya shilingi 750 kwa safari.
Wakiongea na waandishi wa habari wamesema nauli hiyo ya shilingi elfu moja ni ya mpito na ilitangazwa mwezi Agosti mwaka huu na ilitakiwa ianze kutumika baada ya watoa huduma kuitangaza kwa siku 14 kabla ya kuanza kuitumia.
"Nauli hiyo ni kianzio tu ili kuwawezesha wawekezaji kuanza kutoa huduma na si mwisho bali ipo kwa ajili ya kuangalia kama itafaa kuendelea kutumika kulingana na uhalisia" Alisema Dkt. Suluo
Aidha, ili nauli ya kudumu kutangazwa kanuni zinahitaji DART ifanye maombi ya nauli kwa mujibu wa Sheria na utaratibu kukamilika ikiwa ni pamoja na kupokea maoni ya wadau na kuchambua gharama za utoaji huduma hiyo.
Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Dart Said Tunda amesema kuwa nauli ya shilingi 1,000 inafaa kwa kuanzia ili kuhakikisha abiria wanapata huduma bora na endelevu kwani wakati huduma za BRT hazipo, wananchi walikuwa wanatozwa hadi shilingi 6,000 kwa safari kwa vyombo vidogo vya usafiri.