NJOMBE:ADAIWA KUUA MKE KWA SUMU AKIMUWAHI BAADA YA KUHISI YEYE KUWEKEWA KISHA NAYE AJINYONGA
Dec 29, 2025•Channel
AI Analysis
Data from YouTube Data API v3•Updated Just now
Video Overview
Video Details
Published6 months ago
Duration0:06
Video ID3gdA5lK-pPE
Languagesw
CategoryNews & Politics
PrivacyPublic
Made for KidsNo
Video TypeYouTube Short
Performance Metrics
Views19.6K
Likes295
Comments3
Engagement Rate1.52%
Likes per 100 views1.50
Comments per 1K views0.15
Description
Watu watatu wa familia moja katika kijiji cha Kifumbe halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamekutwa wamefariki huku chanzo kikidaiwa kuwa ni sumu pamoja na kujinyonga kutokana na ujumbe ulioachwa na marehemu.
Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe limethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kubainisha kuwa waliokutwa wamefariki usiku wa kuamkia December 29 ni pamoja na Meshack Chagavalya (23) Mke wake Elizabeth Msigwa (25) pamoja na Sara Msuluja (2) ambaye ni mtoto wa kiume wa kambo waliyekuwa wakiishi naye.
Polisi imesema chanzo cha vifo hivyo kwa mujibu wa uchunguzi wa awali ni kuwa,Ujumbe uliopatikana kwenye simu huyo mwanaume (Marehemu) aliomtumia baba yake akimwomba msamaha kuwa aliamua kumwekea sumu kwenye chakula mke wake baada ya kuhisi kuwa mke wake amemuwekea sumu kwenye chakula hivyo akamuwahi.
Aidha baada ya kumwekea sumu mke wake uchunguzi unaonyesha alimnyonga mtoto wake wa kambo na kamba ya manila kwa kimtundika kwenye kenchi.
Baada ya kufanya hivyo naye alijinyoga kwa kamba ya manila kwa kujitundika juu ya kenchi ndani ya chumba walichopanga.