DCEA YANG’ARA KIMATAIF YASHINDA TUZO
Dec 5, 2025•Channel
AI Analysis
Data from YouTube Data API v3•Updated Just now
Video Overview
Video Details
Published5 months ago
Duration1:45
Video IDVFDwUT3KCss
Languagesw
CategoryPeople & Blogs
PrivacyPublic
Made for KidsNo
Video TypeRegular Video
Performance Metrics
Views97
Likes0
Comments0
Engagement Rate0.00%
Likes per 100 views0.00
Comments per 1K views0.00
Description
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa Tuzo ya Umahiri katika Utayarishaji Bora wa Taarifa za Hesabu kwa mwaka 2024, kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu (IPSAS) katika kundi la Taasisi za Serikali zinazojitegemea.
Tuzo hiyo imetolewa tarehe 04/12/2025 na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha NBAA APC Hotel, Bunju jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amepongeza Kitengo cha Fedha na Uhasibu kwa kufanikisha uandaaji bora wa hesabu uliopelekea ushindi huo.
“Niwashukuru watumishi wote wa Mamlaka, hususan timu ya fedha na ukaguzi wa ndani kwa kujitoa, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha taarifa zetu za fedha zinaandaliwa kwa kiwango cha juu kinachotambulika kimataifa. Tuzo hii ni matokeo ya kazi yao, nidhamu na ushirikiano ndani ya taasisi,” amesema Kamishna Jenerali Lyimo.
Ameongeza kuwa ushindi huo ni uthibitisho kuwa DCEA inazingatia kikamilifu sheria za fedha, manunuzi pamoja na miongozo inayotolewa na Hazina kwa nyakati tofauti.
Amesema, “DCEA inazingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za umma inayotolewa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Ni heshima kubwa kutambuliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).”
Aidha, amesema tuzo hiyo ni chachu ya kuongeza bidii katika kudumisha uwazi, uadilifu na usimamizi bora wa rasilimali.
Hii ni mara ya nane kwa DCEA kushinda tuzo hizo tangu mwaka 2017, na Mamlaka imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Watanzania wote.